BUKOBA SPORTS

Saturday, February 21, 2015

KILUVYA FC YA PWANI YASHINDWA KUHIMILI MIKIKI YA RED ARROWS YA ZAMBIA, YAPIGWA 3-0.

TIMU ya Kiluvya FC, ya Pwani imejikuja ikipokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Red Arrows ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam juzi.
Kiluvya FC ambao wanaongoza Ligi Daraja la pili bila kufungwa walijikuta wakipokea kipigo hicho toka kwa wageni hao ambao wanacheza ligi Kuu ya Zambia ambao wapo nchini kujiandaa na Ligi yao.


Jahazi la Kiluvya lilianza kuzama dakika ya 27 baada ya mshambuliaji Testus Mbwewe kufunga bao kwa ustadi kwa kuwazidi mbio mabeki wa Kiluvya hali iliyowafanya kuzinduka na kuanza kushambulia lakini walijikuta wakienda mapumziko bila kubadili matokeo hayo.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Red Arrows walitoa wachezaji saba na kuingiza wengine saba hali iliyozindisha umakini kwani dakika ya 53 mshambuliaji Brenson Chama aliongeza bao la pili baada ya kipa wa Kiluvya FC kutema mpira na yeye kuutia wavuni bila ajizi.
Timu ya Red Arrows
Timu ya Kiluvya FC

Benchi la Red Arrows
Waamuzi na manahodha wa mchezo
Benchi la Kiluvya Fc
Baada ya bao hilo Kiluvya walijitahidi kuanzisha mashambulizi lakini ukuta wa Red Arrows uliojengwa na wachezaji wenye miili mikubwa na warefu wa kimo ulikuwa kikwazo kwao kwani ulikuwa haupitiki.
Red Arrows walionekana kumiliki mpira huku pasi zao zikiwa za haraka haraka walifanya shambulizi dakika ya 75 na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na mshambuliaji wa Daniel Sibanda baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Kiluvya wakidhani ameotea.

Baada ya mchezo huo kocha wa Red Arrows Mathew Phiri, alisema kikubwa anachojengwa kwa wachezaji wake ni mchezo wa kushirikiana na pasi za haraka hivyo mechi za kirafiki zitasaidia kupima uchezaji wa kila mchezaji.
“Tumeweka kambi Tanzania ili wachezaji waone mazingira mapya ambayo yatakuwa yakiwafanya akili kutulia ili ninachofundisha wakielewe zaidi kuliko wangekuwa kwenye mazingira yaleyale ya siku zote”, alisema Phiri
Naye kocha wa Kiluvya FC, Yahaya Issa alisema matokeo ya kufungwa wanayachukulia kama changamoto kwao pia alisema wachezaji wake waliogopa mechi na walikuwa wakichelewa kutoa pasi jambo lilisababisha kupoteza pasi kwani wapinzani walikuwa wepesi kujipanga kuzuia wakipoteza mpira.

No comments:

Post a Comment