BUKOBA SPORTS

Sunday, February 15, 2015

LA LIGA: BARCELONA 5 -0 LEVANTE, LIONEL MESSI KAMA KAWA!! AFUNGA HAT-TRICK, SUAREZ ALIONA LANGO NAE TENA!

Barcelona wakiwa kwao Nyumbani Nou Camp leo jumapili waliichapa Levante Bao 5-0, huku Lionel Messi akipiga Hetitriki, na kuwakaribia Vinara wa La Liga Real Madrid na sasa wapo Pointi 1 nyuma yao.
Hadi Mapumziko, Barca walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao za Neymar, Dakika ya 17, na Lionel Messi, Dakika ya 38.
Kipindi cha Pili, Messi aliongeza Bao 2, moja la Penati, na Luis Suarez kupiga 1 na kuwatwanga Levante Bao 5-0.
Wachezaji wa Barca wakipongezana..Suarez na MessiNeymar akifukuziwa na wachezaji wa Levante hii leo

No comments:

Post a Comment