LA LIGA: BARCELONA 3 vs 2 VILLARREAL, MESSI AIPA USHINDI BARCA, SASA KWENYE MBIO SAMBAMBA NA REAL!
3-2 VILLARREAL bao zao zilifungwa dakika ya 30 na D. Cheryshev na bao la pili L. Vietto. Lionel Messi alifunga Bao la ushindi usiku huu Uwanjani Nou Camp wakati Barcelona inatoka mara mbili nyuma na kuifunga Villareal Bao 3-2 katika Mechi ya La Liga. Sasa Barca wako Pointi 1 nyuma ya Vinara Real Madrid lakini Barcelona wamecheza Mechi 1 zaidi. Barca walijikuta wako nyuma kwa Bao la Dakika ya 30 la Denis Cheryshev lakini Neymar akarudisha Dakika ya 45 na Luciano Vietto kuwapeleka Villareal mbele kwa mara ya Pili kwa Bao la Dakika 51.
Kisha Rafinha Alacantara akaisawazishia Barca Dakika ya 53 na Lionel Messi kupiga Bao la ushindi katika Dakika ya 55.
No comments:
Post a Comment