BUKOBA SPORTS

Saturday, February 7, 2015

FULL TIME: ATLETICO MADRID 4 vs 0 REAL MADRID. REAL HOI LEO!! ACHINJWA BILA KUJITETEA UGENINI ESTADIO VICENTE CALDERON!!

Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia baada ya kuichapa bao la pili kipindi cha kwanza Real Madrid. Bao la kwanza likifungwa na Tiago dakika ya 14 na bao la pili lilifungwa na Saúl katika dakika ya 18' kwenye Uwanja wao wa nyumbani Estadio Vicente Calderón, Madrid. Mtanange unaochezeshwa
na Mwamuzi David Fernandez Borbalan. 

A. Griezmann aliwamaliza nguvu Real pale alipofunga bao la tatu katika dakika dakika ya 67 na  M. Mandžukić aliwapiga bao la mwisho la nne dakika ya lala salama dakika ya 89 na kufanya 4-0 dhidi ya Real Madrid.

Wachezaji wa Atletico wakishangilia moja ya bao lao.
VIKOSI:
Atletico Madrid:
Moya, Juanfran, Godin, Miranda, Siqueira, Gabi, Tiago, Koke, Arda, Griezmann, Mandzukic.
Akiba: Oblak, Gamez, Gimenez, Mario, Saul, Raul Garcia, Torres.

Real Madrid: Casillas, Varane, Nacho, Coentrao, Carvajal, Khedira, Kroos, Isco, Bale, Ronaldo, Benzema.
Akiba: Navas, Hernandez, Lucas Silva, Arbeloa, Jese, Llorente, Illarramendi.

No comments:

Post a Comment