Hadi Mapumziko Real waliongoza kwa Bao la Dakika ya 22 la Isco aliefunga baada ya Krosi ya Garreth Bale kumkuta Karim Benzema alieisindikiza Golini na Ronaldo kushindwa kuunganisha na Mpira kumkuta pembeni Arbeloa ambae aliurudisha nyuma na Isco kuachia Shuti lililotinga Wavuni.
Bao la Pili la Real lilifungwa Dakika ya 73 na Karim Benzema.
Nyota wa Real, Ronaldo na Garreth Bale, walikosa Mabao wakati Mashuti yao mawili yalipopiga Posti.
Hii Leo Barcelona watakuwa Nyumbani Nou Camp kucheza na Levante na Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, ambao wako Pointi 7 nyuma ya Real, wako Ugenini kucheza na Celta Vigo.

No comments:
Post a Comment