Majuzi Jumatano Villa ilimtimua Meneja wao Paul Lambert baada ya kwenda Mechi 10 za Ligi Kuu England bila ushindi na kufunga Bao 2 tu katika Mechi hizo.
Tim Sherwood, mwenye Miaka 46, alifanya kazi yake ya mwisho kama Meneja wa Tottenham alipombadili Andre Villas-Boas Desemba 2013 lakini akatimuliwa mwishoni mwa Msimu uliopita na amekuwa hana kibarua tangu wakati huo.

Akiwa kama Mchezaji, Sherwood, ambae aliichezea England mara 3, alijiunga na Tottenham Mwaka 1999 kutoka Blackburn Rovers ambako akiwa kama Nahodha waliweza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu wa 1994/5.
No comments:
Post a Comment