
Habari inawadia wakati the Gunners wanajiandaa kukabiliana na Manchester United, kuwania taji la FA katika hatua ileile walioambulia kichapo cha 4-0 katika msimu wa mwaka wa 2008.
"Ni wazi iwapo ratiba ya mechi ya FA imewekwa karibu sana na mechi za kuwania ubingwa wa bara ulaya kama kocha ni wajibu wao kubaini ipi kati ya mechi hizo ni muhimu.'' alisema Wenger.
''kama unawachezaji wazuri unawapumzisha na badala yake kuwachezesha wengine katika mchuano wa FA.
Hawatakuwa na mechi nyengine hadi tarehe 17 mwezi huu na hivyo huenda ikamruhusu Wenger ama Professa Wenger kuwachezesha nyota wake wa kutegemewa bila ya hofu ya kuwapoteza kwa majeraha.
Kocha wa Man united
Iwapo hali ni shwari Wenger huenda akawania ushindi wake wa kwanza uwanjani old Trafford tangu mwaka wa 2006.
Wenger anaamini kuwa matokeo ya mechi hiyo ya FA itaisaidia Arsenal kubaini kasi yake katika uwaniaji wa nafasi nne bora katika ligi kuu ya Premia.
Arsenal inaalama moja pekee mbele ya United ambayo inashikilia nafasi ya nne katika jedwali la ligi kuu ya Premia ya Uingereza.
Wenger "mechi ya jumatatu itakuwa mechi ya kukata na shoka maanake iwapo timu inashinda mechi kubwa na yenye hadhi kama hii wachezaji wake huwa wanaimarika kisaikolojia na motisha wao unawasaidia kushinda mechi zaidi''
No comments:
Post a Comment