BUKOBA SPORTS

Monday, March 30, 2015

MANCHESTER UNITED MSIMU HUU IKIMALIZA NDANI YA 4 BORA, KOCHA WAKE VAN GAAL KUZOA BONASI £1M

Kocha wa Man United  Louis van Gaal endapo atafanikiwa kuiingiza Manchester United kwenye 4 Bora ya Ligi Kuu England na hivyo kufuzu kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao, basi atavuna Pauni Milionin1 kama Bonasi yake.
Mara alipokabidhiwa Umeneja mwanzoni mwa Msimu huu, Van Gaal alielekezwa 4 Bora ndio lengo la chini kwa Man United na ili kumpa motisha akawekewa hiyo Bonasi.
Msimu uliopita, Man United chini ya David Moyes aliefukuzwa, walimaliza Nafasi ya 7 kwenye Ligi na kukosa kucheza Ulaya na hilo limeathiri mapato yao na pia kuvuruga mwonekano wao kama moja ya Klabu kubwa Duniani.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya 5 Liverpool huku Mechi zikibakia 8 Msimu kumalizika.

No comments:

Post a Comment