Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa Mchezaji wao Raheem Sterling hakuonyesha nidhamu ya Mwanamichezo baada ya kuibuka Picha akivuta Mtemba maarufu kama Shisha ambao unadhaniwa kuwa na Gesi inayolewesha 'Nitrous Oxide.'
Picha za Sterling akivuta Shisha zilizagaa Jana huko England kwenye Vyombo vya Habari na baadae kuibuka Picha nyingine zikimwonyesha Staa huyo wa Miaka 20 ambae pia huchezea England akiwa 'amezimika.' Akiongea mara baada ya Jana Liverpool kuifunga Newcastle 2-0 na kupanda hadi Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England huku Sterling akifunga Bao la kwanza, Rodgers amesema: "Ukiwa Mwanamicheza wa kiwango cha juu hupaswi kufanya hivyo. Nitaongea nae na kumsikia anasemaje."
Rodgers amekiri kuwa Wachezaji Vijana Siku zote hufanya makosa lakini kikubwa ni kujifunza toka makosa hayo.
Hata hivyo Rodgers amesisitiza kuwa Adhabu yeyote itakayotolewa itakuwa ni kitu cha ndani ya Klabu.
Hivi sasa Sterling na Liverpool ziko kwenye mvutano baada ya Staa huyo kugomea kusaini Mkataba mpya huku kukiwa na tetesi yuko mbioni kuhamia Klabu kubwa Ulaya huku Real Madrid, Barcelona, Chelsea na Arsenal zikitajwa kuwa zinamlenga.
Baada ya kuibuka tetesi hizo Liverpool ilidai Sterling haendi popote na kusema mazungumzo ya Mkataba mpya yataendelea mwishoni mwa Msimu.
No comments:
Post a Comment