BUKOBA SPORTS

Monday, April 20, 2015

KLABU YA PSV EINDHOVEN YAWEKA WAZI MCHEZAJI WAO KUTAKWA NA MANCHESTER UNITED MEMPHIS DEPAY.

Mabingwa wapya wa Holland, PSV Eindhoven, wametoboa kuwa Manchester United imewafuata kuulizia kupatikana kwa Fowadi wa Klabu hiyo Memphis Depay.
Memphis Depay ndie Mfungaji Bora wa Ligi ya Holland, Eredivisie, akipachika Bao 20 ambazo zimeiwezesha PSV kutwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza katika Miaka 7.
Mkurugenzi wa Ufundi wa PSV, Marcel Brands, akiongea na Kituo cha TV cha Holland, ameeleza: “Tumepokea Simu inayoulizia kuhusu Mchezaji huyo. Lakini mazungumzo hayajaanza. Klabu kadhaa kubwa zinamwania!”
Juzi Jumamosi, Depay, ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya Holland, aliifungia PSV Bao la Pili walipoifunga Heerenveen Bao 4-1 na kutwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza tangu 2008.
Brands amesema Dau la kumnunua Depay ni zaidi ya Pauni Milioni 14.4 ambazo Mwaka Jana Tottenham walitoa Ofa iliyokataliwa ya kumnunua.
Brands amefafanua: “Ili kumnunua, Ofa iwe ni zaidi ya Tottenham. Huyu ni Mchezaji ghali.”
Nae Kocha wa PSV Phillip Cocu amesema anategemea Depay na Kiungo wao Georginio Wijnaldum wataihama Klabu yake.
Mwaka Jana, Depay aling’ara huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia wakati Holland ilipomaliza wakiwa Washindi wa Tatu chini ya Kocha Louis van Gaal ambae mara baada ya Fainali hizo alihamia Manchester United kuwa kama Meneja wao.

No comments:

Post a Comment