BUKOBA SPORTS

Saturday, April 25, 2015

FULL TIME: SOUTHAMPTON 2 vs 2 TOTTENHAM HOTSPURS


BAO za Southampton
Graziano Pellé 29

Graziano Pellé 65

2 - 2
BAO za Tottenham Hotspur Erik Lamela 43, Nacer Chadli 70


Tottenham ilitoka nyuma mara mbili na kuambua Sare ya Bao 2-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyozikutanisha Timu ambazo zinafuatana kwenye Msimamo wa Ligi.
Southampton walitangulia kufunga kwa Bao la Mtaliana Graziano Pelle Dakika ya 29 na Erik Lamela kusawazisha Dakika ya 43.
Kipindi cha Pili Dakika ya 65 Pelle tena aliwapeleka Southampton mbele na Nacer Chadli kuisawazishia Tottenham Dakika ya 70.
Matokeo haya yameibakisha Tottenham nafasi ya 6 Pointi 1 mbele ya Southampton ambao wako nafasi ya 7.

VIKOSI:
Southampton:
Kelvin Davis, Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand, Schneiderlin, Alderweireld, Ward-Prowse, Mane, Steven Davis, Pelle
Akiba: Gardos, Long, Tadic, Elia, Gazzaniga, Reed, Targett

Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Fazio, Vertonghen, Davies, Mason, Bentaleb, Lamela, Eriksen, Chadli, Kane
Akiba: Chiriches, Soldado, Yedlin, Vorm, Townsend, Dembele, Stambouli
Refa: Jonathan Moss

No comments:

Post a Comment