BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 5, 2015

BAYERN MUNICH WAFANYA MAZOEZI MAKALI KUKABILIANA NA BARCELONA UEFA CHAMPIONS LEAGUE. LEWANDOWSKI KUVAA KINGA (MASK) USONI WAKATI WA MECHI!

Nusu Fainali nyingine ya UCL ni Jumatano huko Nou Camp Mjini Barcelona Nchini Spain, ambapo Wenyeji Barcelona wanaoongoza La Liga, watawakaribisha Mabingwa wa Germany Bayern Munich ambayo sasa ipo chini ya Kocha Pep Guardiola ambae alijizolea sifa kubwa kwa kutwaa Mataji kibao akiwa na Barcelona kabla kung'atuka Miaka michache iliyopita. Marudiano ya Nusu Fainali hizi za UCL yatafanyika Wiki ijayo Jumanne na Jumatano, Mei 12 na 13.

Meneja wa Bayern Munich  Pep Guardiola akiteta na jambo wakati wa Mazoezi yao kujiandaa na kipute cha kukata na shoka kati yao na Barcelona kesho Jumatano kwenye Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League.

Robert Lewandowski akiwa amevaa Mask kujilinda na kesho anategemea kuvaa kwa ajili ya kujilinda kuumia zaidi wakati wa Mtanange huo wa kwanza.

Guardiola anarudi kuiwinda Timu yake ya Zamani mwaka 2008 na 2012 na sasa anarudi kukutana nayo uso kwa uso kwa mara nyingine huku wakionekana kuwa Bayern kuwa na Ubabe zaidi ya Barca kitu kinachofanya Baadhi ya Mashabiki kuona itakuwa ni Shughuli pevu.

No comments:

Post a Comment