BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 5, 2015

KOCHA JOSE MOURINHO AMNYOOSHEA MIKONO JUU SIR ALEX, ADAI REKODI YAKE NI NGUMU KUIFIKIA! AMWAGIA SIFA MZEE FERG!

Jose Mourinho ameungama kutoifikia Rekodi ya Sir Alex Ferguson ya kutwaa Mataji 13 ya Ligi Kuu England na kukiita ni kitu 'kisichowezekana.'
Jumapili, Jose Mourinho aliiongoza Chelsea kutwaa Ubingwa wake wa 3 wa Ĺigi Kuu England akiwa na Klabu hiyo baada ya kuifinga Crystal Palace 1-0.
Sir Alex alikuwa na Miaka 51 alipoanza kuiongoza Manchester United kutwaa Taji la kwanza la Ligi Kuu England Msimu wa 1992/93 na kuendelea kubeba mengine 12 baada ya hapo.
Hivi sasa Mourinho ana Miaka 52 na pamoja na Taji la Msimu huu alishatwaa Mataji mengine mawili akiwa na Chelsea katika kipindi chake cha kwanza katika Misimu ya 2004/05 na 2005/06.
Akiongea na BT Sport, Mourinho alisema: "Nina safari ndefu ya kwenda lakini Sir Alex ameacha kiwango cha juu ambacho hakiwezekani kwa yeyote. Siwezi kutwaa Mataji 13 ya Ligi Kuu England!"
Aliongeza: "Naweza kutwaa Ubingwa mara 13. Naweza. Ninayo Mataji 8. Naweza kufikia 13. Lakini Mataji 13 ya Ligi Kuu England, hapana, haiwezekani!"
Mourinho ameshatwaa Ubingwa huko Portugal mara 2 akiwa na FC Porto, mara 2 huko Italy akiwa na Inter Milan, mara 1 Nchini Spain akiwa na Real Madrid na hizi 3 za Chelsea.
Jose ameiongoza Chelsea kubeba Ubingwa wa msimu huu wa 2014/2015

No comments:

Post a Comment