Baada kukosa Penati iliyookolewa na Kipa, Kepteni wa Liverpool, Steven Gerrard, alifuta makosa yake na kuipa Bao la ushindi Liverpool walipoifunga Timu ambayo iko kwenye balaa kushushwa Daraja, QPR, Bao 2-1.
Liverpool, wakiwa kwao Anfield, walitangulia kufunga katika Dakika ya 19 kwa Bao la la Philippe Coutninho na QPR kusawazisha Dakika ya 73 Mfungaji akiwa Leroy Fer.
Liverpool walipewa Penati Dakika ya 79 na Gerrard kuikosa na kisha Dakika ya 82 QPR kubaki Mtu 10 baada ya Nedum Ohuoha kupewa Kadi za Njano 2 ndani ya Dakika 3 tu na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 87, Gerrard akafunga Bao la ushindi kwa Liverpool na kuweka hai matumaini yao finyu ya kufuzu 4 Bora wakiwa Nafasi ya 5 Pointi 4 nyuma ya Man United wenye Mechi 1 mkononi huku Liverpool wakibakiza Mechi 3.
No comments:
Post a Comment