BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 26, 2015

RADAMEL FALCAO KURUDI MONACO


Radamel Falcao Amefunga bao nne tu kwenye msimu wa 2014-2015 Ligi Kuu England akiwa na Manchester United akicheza kwa mkopo katika Klabu hiyo.
KLABU ya Manchester United imefikia uamuzi wa kumuacha Radamel Falcao kufuatia kumaliza mkopo wake akitokea Monaco. Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia ambaye alikosa mchezo wa Jumapili hii wa sare ya bila ya kufungana na Hull City kwasababu ya majeruhi, ameifungia United mabao manne katika mechi 29 alizocheza. Kutoka na hilo United imeamua kutomnunua moja kwa moja Falcao mwenye umri wa miaka 29 kama ilivyokuwa katika makubaliano yao mwanzoni. Meneja wa United Louis van Gaal alithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa klabu na kumtakia kila la heri nyota huyo popote aendapo. Mara ya mwisho Falcao kuifungia United ilikuwa katika mchezo dhidi ya Leicester City Januari 31 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment