Lionel Messi kulia akiachia shuti kali.
Nao Mabingwa Watetezi Uruguay wametinga Robo Fainali za Copa America kwa Tiketi ya moja ya Timu mbili zilizofuzu Nafasi ya 3 Bora katika Kundi lao baada ya kutoka Sare 1-1 na Paraguay ambao wameshika Nafasi ya Pili ya Kundi B.
Argentina, ambao Jana waliitungua Jamaica, Timu ambayo ni Wageni Waalikwa wa Mashindano haya, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 11 la Gonzalo Higuian, wao wameshika Nambari Wani Kundi B.
Katika Mechi ya Uruguay na Paraguay, Bao la Dakika ya 29 la Jose Maria Gimenez liliwapa Uruguay uongozi lakini Dakika ya 44 Lucas Barrios aliisawazishia Paraguay.
No comments:
Post a Comment