BUKOBA SPORTS

Monday, June 22, 2015

COPA AMERICA: BRAZIL 2 vs 1 VENEZUELA, THIAGO SILVA NA ROBERTO FIRMINO WAIPA USHINDI BRAZIL NA KUSONGA HATUA YA ROBO FAINALI.

Kipindi cha pili dakika ya 51 Roberto Firmino aliwawezesha Brazil kwa kufunga bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Venezuela akipata pasi safi kutoka kwa Willian na kuumalizia nyavuni.Wakipongezana Brazil kwa ushindi Bao la Venezuela lilifungwa dakika ya 84 kupitia kwa Miku na kufanya bao kuwa 2-1. Mechi hii Brazil walicheza bila Nahodha wao Neymar ambaye ameuangalizia mtanange huu jukwaani kama shabiki baada ya kuoneshwa kadi nyekundu na kufungiwa mechi nne kwa utovu wa nidhamu.1-0 Thiago Silva anaifungia bao BrazilThiago Silva aliwafungia bao la kuongoza Brazil dakika ya 9 baada ya kupigwa kona na Robinho kufanikisha bao hilo kufungwa na Silva kwa kuunganisha mpira moja kwa moja ndani ya lango la Venezuela.
Mtanange unaofuata punde wa Copa America ni kati ya Brazil vs Venezuela kwenye Uwanja wa Estadio Monumental David Arellano, Santiago de Chile Ukiongozwa na Mwamuzi E. CáceresVIKOSI:
  • Venezuela bench: Hernandez, Farinez, Angel, Martinez, Acosta, Perozo, Murillo, Gonzalez, Lucena, Rivas, Miku.
  • Venezuela (4-2-3-1): Baroja; Rosales, Tunez, Vizcarrondo, Cichero; Rincon, Seijas; Guerra, Arango, Vargas; Rondon.
  • Brazil bench: Neto, Marcelo Grohe, Fabinho, Marquinhos, David Luiz, Geferson, Casemiro, Fred, Douglas Costa, Everton Ribeiro, Diego Tardelli.
  • Brazil (4-2-3-1): Jefferson; Dani Alves, Thiago Silva, Miranda, Filipe Luis; Fernandinho, Elias; Willian, Coutinho, Robinho; Firmino.

No comments:

Post a Comment