BUKOBA SPORTS

Tuesday, July 28, 2015

JEZI MPYA ZA SIMBA SPORTS CLUB KWENYE DUKA LA MTANDAO JUMIA

KLABU ya Simba kwa kushirikiana na Kampuni ya kuuza vitu kwa njia ya Mtandao ‘Jumia’ wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015-2016 ‘Jumia – Simba Online Shop’ kupitia katika duka la mtandao la Jumia Iiitwayo la www.jumia.co.tz.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema dhumuni la huduma hiyo ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo nchini.
Aveva alisema klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake vya michezo nchi nzima, hivyo mkataba huo abu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake vya michezo nchi nzima, hivyo mkataba huo utaongeza usaambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu hiyo.
“Klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa za Simba kiurahisi na kwa bei nafuu” alisema Aveva.
Meneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul alisema uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba.

Alisema katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu huo, kupitia njia ya mtandao hivyo wanajivunia kwa Aveva kuwachagua wao kwa kazi hiyo.
“Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia leo(jana) mpaka Alhamisi Julai 31 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa rasmi kwa rejareja”.



“Tunawahamasisha wapenzi wa Simba popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitia mtandao huu, kuona urahisi katika kufanya manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaweza kuagiza jezi kupitia tovuti ya jumia na kuletewa mzigo wako mpaka mlangoni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited, Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongeza mapato yake pia kudhibiti bidhaa feki,”.

No comments:

Post a Comment