BUKOBA SPORTS

Sunday, July 19, 2015

KAGAME CUP 2015: AZAM FC 1 - 0 KCCA, NAHODHA JOHN BOCCO IPA USHINDI AZAM


Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli pekee lililofungwa na John Bocco dhidi ya KCCA ya Uganda katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshabuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche (kulia) akichuana na beki wa KCCA ya Uganda, Wasswa Hassan katika mchezo wa Kombe la Kagame.

Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (katikati) akitafuta mbinu za kumtoka kipa wa KCCA ya Uganda, Ochan Benjamin katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 1-0.

AZAM FC imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuwafunga KCCA ya Uganda bao 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mfungaji wa bao hilo la pekee ni Nahodha, John Raphael Bocco Kipindi cha kwanza na Kipindi cha pili hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake.


Hekaheka katika lango la KCCA

No comments:

Post a Comment