BUKOBA SPORTS

Monday, July 13, 2015

MANCHESTER UNITED YATAMBULISHA WAPYA 3 KWA MPIGO LEO, TAYARI KWA ZIARA KWENDA MAREKANI!


Bastian SchweinsteigerEmbedded image permalink
Morgan Schneiderlin nae katambulishwa rasmi hii leo
Jana Viungo, Morgan Schneiderlin toka Southampton na Bastian Schweinsteiger wa Bayern Munich, walikuwa wakipitia utaratibu wa kupimwa Afya zao na Leo watakuwa ndani ya Ndege pamoja na Kikosi kizima cha Man United kwenda Marekani kuanza Ziara yao.
Man United tayari imeshanunua Wachezaji Wawili, Memphis Depay toka PSV Eindhoven na Mchezaji wa Torino Matteo Darmian. 


Wakati Man United wakinunua wapya, Straika wao Robin van Persie amehamia huko Uturuki na kujiunga na Fenerbahce akiungana na Winga Nani alieuzwa huko Wiki iliyopita.
Kuuzwa kwa Van Persie kunaiacha Man United ikiwa na Mastraika Wawili tu wanaotambulika, Kepteni Wayne Rooney na Chipukizi James Wilson.
Huko Marekani, Man United watacheza Mechi 4 dhidi ya Club America ya Mexico, San Jose Earthquakes ya Marekani, FC Barcelona na PSG.
Man United watafungua Msimu mpya wa Ligi Kuu England hapo Agosti 8 kwa kucheza Old Trafford na Tottenham.
Pia, Mwezi Agosti, Man United wanahitajika kucheza Raundi ya Mchuujo ili kufuzu kucheza Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI na watabaini Mpinzani wao hapo Agosti 7 wakati Droo yake itakapofanywa na UEFA.

No comments:

Post a Comment