BUKOBA SPORTS

Monday, July 20, 2015

UHAMISHO: KIPA SERGIO ROMEO ATAKIWA OLD TRAFFORD!

Manchester United wananyemelea kumsaini Kipa Sergio Romero wakati Meneja wao, Louis van Gaal, akisaka kumbadili Victor Valdés anaeuzwa.
Romero, mwenye Miaka 28, Msimu uliopita alikuwa kwa Mkopo huko AS Monaco kutoka Sampdoria na kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka Jana, Kipa huyo aling'ara alipokuwa Namba Wani wa Argentina iliyofika Fainali na kufungwa 1-0 na Germany.
Hata hivyo, AS Roma nayo pia inamtaka Romero ambae sasa ni Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake na Sampdoria kumalizika.
Van Gaal anamtaka Romero kuziba pengo la Valdés ambae alikwaruzana nae kwa kugomea kuchezea Kikosi cha Pili cha Man United na hilo kumfanya asichukuliwe kwenye Ziara ya sasa huko Marekani.

Man United pia ina uwezekano wa kumpoteza Kipa wao Namba Moja, David de Gea, anaetakiwa kwa udi na uvumba na Klabu ya Nchini kwao Spain, Real Madrid.
Hata hivyo, Sergio Romero anatarajiwa kuwa Kipa Namba Mbili nyuma ya Kipa yeyote atakaembadili De Gea, ikiwa ataondoka, huku Kipa wa Ajax na Timu ya Taifa ya Holland, Jasper Cillessen, akitajwa kuwa ndie mrithi wa De Gea.

No comments:

Post a Comment