Kepteni wa England na Manchester United Wayne Rooney Usiku huu ameandika Historia mpya kwa Nchi yake baada ya kufunga Bao lake la 50 na kumfanya awe ndie Mfungaji Bora katika Historia ya Nchi hiyo wakati England inaichapa Switzerland 2-0 Uwanjani Wembley Jijini London katika Mechi ya Kundi E la EURO 2016.
Ijumaa iliyopita, Rooney alifunga Bao 1 kwa Penati wakati England inaifunga San Marino 6-0 katika Mechi ya Kundi E la EURO 2016 na kumfikia Sir Bobby Charlton ambae ndie alikuwa akishikilia Rekodi ya Ufungaji Bora kwa England aliyoiweka Mwaka 1970 kwa kufunga Bao 49 kwa Mechi 106 tangu aanze kuichezea England Mwaka 1958.
Leo tena Rooney alifunga Bao la Pili kwa Penati na kufikisha Bao 50 katika Mechi 106 ukiwa ni Mwaka wa 12 tangu aifungia England Bao lake la kwanza na kuivunja Rekodi ya Miaka 45 iliyowekwa na Sir Bobby Charlton.
Katika Mechi hii na Switzerland, Bao la kwanza la England lilifungwa na Harry Kane katika Dakika ya 67 na Rooney kufunga la pili Dakika ya 84.
Kabla ya Mechi hii England walikuwa tayari wamefuzu kucheza Fainali za EURO 2016 Mwakani huko France huku wakiwa na Mechi 3 mkononi.
No comments:
Post a Comment