BUKOBA SPORTS

Friday, September 11, 2015

KIPA DAVID DE GEA ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE NA KLABU YA MANCHESTER UNITED.

Hatimaye kipa wa Namba moja wa Manchester United amesaini mkataba wa miaka 4 na Klabu ya Mashetani wekundu leo.
Real Madrid kushindwa kumsaini David De Gea katika Dakika za mwisho za Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho hapo Agosti 31, Kipa huyo wa Spain ameamua kusaini Mkataba mpya na Klabu yake Manchester United. Old Trafford Leo imethibitisha, De Gea, ambae Mkataba wake ulikuwa ukiisha Juni Mwakani, sasa amesaini Mkataba mpya wa Miaka Minne na Man United.

Kipa huyo amekuwa ndio chaguo la Washabiki wa Man United kuwa ndie Mchezaji Bora wa Klabu kwa Miaka Miwili iliyopita lakini Msimu huu hajaidakia hata Mechi moja baada ya Meneja Louis van Gaal kumtoa Kikosini akisisitiza sakata la kuhamia Real limemfanya asiwe katulia.
Katika Mechi 6 za Man United za Msimu huu mpya, Kipa wa Kimataifa wa Argentina, Sergio Romero, ambae alihamia Man United Mwezi Agosti, ndie amekuwa akidaka.
Lakini baada ya sakata lake kumalizika vizuri inaaminika Van Gaal Jumamosi atampanga De Gea, ambae Juzi aliidakia Spain wakati wanaifunga Macedonia katika Mechi ya EURO 2016, kuivaa Liverpool Uwanjani Old Trafford katika Mechi ya Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment