BUKOBA SPORTS

Saturday, September 12, 2015

LIGI KUU VODACOM KUANZA KESHO JUMAMOSI SEPT. 12, MSIMU MPYA 2015/2016. SIMBA KUANZA NA SPORTS, YANGA KUWAVAA COASTAL UNION JUMAPILI. KAGERA SUGAR UGENINI MBEYA!

LIGI KUU VODACOM, VPL [Vodacom Premier League], inaanza Jumamosi kwa Mechi 7 na Jumapili Mabingwa Yanga kushuka Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Coastal Union.
Hiyo Jumamosi, Washindi wa Pili wa VPL, Azam FC, wako kwao Azam Complex, huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Saalam kucheza na Prisons wakati Vigogo Simba kusafiri kwenda Mkwakwani, Tanga kuivaa African Sports iliyopanda Daraja Msimu huu.
Mechi nyingine ni Ndanda FC ya Mtwara kuwa wenyeji wa Mgambo Shooting Uwanjani Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa Maafande wa JKT Ruvu katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Stand United FC watawakaribisha Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili VPL itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam ambapo Mabingwa Watetezi Yanga watawakribisha Wagosi wa Kaya Coastal Union.

Wakati huo huo, TFF imetangaza kuwa Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wa Mjini Tabora kwa Mechi zake za Nyumbani dhidi ya Toto Africans (Septemba 26), JKT Ruvu (Septemba 30), Tanzania Prisons (Oktoba 4) na Yanga (Oktoba 31).

Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye Uwanja wao wa Kaitaba Mjini Bukoba unaofanywa na Wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

VPL KUANZA KUTIMUA VUMBI

LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Septemba 12

Ndanda v Mgambo Shooting (Nang’wanda - Mtwara)
African Sports v Simba SC (Mkwakwani - Tanga)
Majimaji v JKT Ruvu (Majimaji - Songea)
Azam FC v Tanzania Prisons (Azam Complex - Dsm)
Stand United v Mtibwa Sugar (Kambarage - Shinyanga)
Toto Africans v Mwadui (CCM Kirumba - Mwanza),
Mbeya City v Kagera Sugar (Sokoine - Mbeya)

Jumapili Septemba 13
Yanga v Coastal Union (Taifa – Dar es salaam).

No comments:

Post a Comment