BUKOBA SPORTS

Wednesday, September 23, 2015

FULL TIME: CELTA VIGO 4 vs 1 BARCELONA, BARCA WAPIGWA KAMA WATOTO LEO! WAUTAFUTA MPIRA KWA TOCHI!!


SPANISH PRIMERA DIVISIÓN 23/9/2015
 Estadio Balaídos, Spain
Mbele ya watazamaji: 23,311 

BAO za Celta Vigo zilifungwa na
Nolito 26' •
Iago Aspas 30' •
Iago Aspas 56' •
John Guidetti 83' •

BAO la Barcelona lilifungwa na Neymar dakika ya 80' 

Estadio Municipal de Balaidos huko Jijini Vigo, umekuwa Uwanja mchungu kwa Mabingwa wa Spain Barcelona walipofungwa Bao 4-1 na Celta Vigo katika Mechi ya La Liga.
Celta Vigo waliongoza 3-0 kwa Bao za Nolito na mbili za Aspas na Barca kufunga Bao moja kupitia Neymar lakini Celta Vigo wakapiga Bao la 4 kupitia John Guidetti.
Hiki ni kipigo cha kwa kwanza kwa Barcelona Msimu huu mpya wa La Liga na ikiwa Mahasimu wao wakubwa Real Madrid watashinda Mechi yao na Athletic Bilbao basi watachukua uongozi.

No comments:

Post a Comment