LEO, katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England huko White Hart Lane, Wenyeji Tottenham Hotspurs waliwachapa Vinara wa Ligi hiyo Manchester City Bao 4-1 na kuhatarisha kupokonywa uongozi wao ikiwa Man United wataifunga Sunderland Leo hii.
City, ambao Wikiendi iliyopita wakiwa kwao Etihad walichapwa 2-1 na West Ham, Leo walitangulia kufunga Bao katika katika Dakika ya 25 kupitia Kevin De Bruyne lakini Eric Dier akaisawazishia Spurs Bao katika Dakika ya 45.
Hapi Mapumziko Spurs 1 City 1.
Kipindi cha Pili, Spurs walicharuka na kupiga Bao 3 kupitia Toby Alderweireld, Harry Kane na Erik Lamela.
Tottenham team
wanaonza XI: Lloris; Walker, Alderweireld, Vertonghen, Davies; Alli, Dier; Eriksen, Son, Lamela; Kane
Akiba: Vorm, Rose, Trippier, Carroll, Chadli, Townsend, Clinton
Manchester City team
Wanaoanza XI: Caballero; Sagna, Demichelis, Otamendi, Kolarov; Fernando, Fernandinho; De Bruyne, Sterling, Toure; Aguero
Akiba: Hart, Kompany, Zabaleta, Nasri, Navas, Roberts, Barker
No comments:
Post a Comment