BUKOBA SPORTS

Sunday, September 13, 2015

VPL-YAANZA: AZAM FC, SIMBA, ZAANZA VYEMA, ZASHINDA! LEO JUMAPILI NI YANGA vs COASTAL TAIFA!

LIGI KUU VODACOM, VPL [Vodacom Premier League], Jana ilianza Msimu mpya wa 2015/16 kwa Mechi 7 ambazo huko Chamazi, Dar es Salaam Azam FC, Timu iliyomaliza Nafasi ya Pili Msimu uliopita, kuitwanga Tanzania Prisons Bao 2-1.
Bao za Mechi hiyo zilifungwa kwa Azam FC zilifungwa na Kipre Tchetche, Dakika ya 39, na Farid Mussa, 81 huku Bao la Prisons likifungwa na Jeremiah katika Dakika ya 60.
Huko Mkwakwani, Tanga, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, African Sports, ilifungwa 1-0 na Simba ambao Bao lao la ushindi lilifungwa na Hamisi Kiiza katika Dakika ya 57. 


Leo Jumapili Mabingwa Yanga kushuka Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Coastal Union.

VPL-LIGI KUU VODACOM
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Septemba 12

Ndanda 1 vs  Mgambo Shooting 1 (Nang’wanda - Mtwara)
African Sports 0 vs Simba SC 1 (Mkwakwani - Tanga)
Majimaji 1 vs JKT Ruvu 0 (Majimaji - Songea)
Azam FC 2 vs Tanzania Prisons 1 (Azam Complex - Dsm)
Stand United 0 vs Mtibwa Sugar 1 (Kambarage - Shinyanga)
Toto Africans 1 vs Mwadui 0 (CCM Kirumba - Mwanza),
Mbeya City 0 vs Kagera Sugar 1 (Sokoine - Mbeya)

Jumapili Septemba 13
Yanga v Coastal Union (Taifa – Dar es salaam).

No comments:

Post a Comment