BUKOBA SPORTS

Sunday, September 13, 2015

LA LIGA: ATLETICO MADRID 1 vs 2 BARCELONA, LIONEL MESSI ATOKA BENCHI NA KUIPA USHINDI BARCELONA.

Lionel Messi amesheherekea kuzaliwa mtoto wake wa pili kwa kutoka Benchi na kuifungia Barcelona Bao la ushindi walipoichapa Atletico Madrid hapo Jana Uwanjani Vicente Calderon Jijini Madrid.
Hilo ni Bao la kwanza kwa Messi kwa Msimu huu mpya wa La Liga baada ya kucheza Mechi 2 bila kufunga.
Lakini hilo ni Bao lake la 287 kwa Barcelona katika La Liga na kumfanya aendelee kuchanja mbuga kama Mfungaji Bora wa Ligi hiyo ya Spain.
Kwenye Mechi hii Atletico ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 51 kwa Bao la Fernando Torres na Barca kusawazisha katika Dakika ya 55 kupitia Neymar.
Messi aliingizwa Dakika ya 60 na katika Dakika ya 77 kupiga Bao la Pili na la ushindi kwa Barca.
Baada ya Mechi 3 Barca wapo kileleni wakiwa na Pointi 9 wakifuatiwa na Real Madrid wenye Pointi 7.

No comments:

Post a Comment