BUKOBA SPORTS

Saturday, October 24, 2015

FULL TIME: WEST HAM UNITED 2 v 1 CHELSEA, NEMANJA MATIC NJE KWA KADI NYEKUNDU! JOSE NAE NJE!! ANDY CARROLL AIFANYIA KITU MBAYA BLUES, AIPANDISHA WEST HAM JUU NAFASI YA PILI!

Carroll akipongezwa na Noble2-1Mkongwe Carroll akipeta kwenye Uwanja wao wa NyumbaniPongeziMeneja wa West Ham nae akishangilia bao la Carroll.
Chelsea Leo wamepokea kipigo chao cha 5 katika Mechi zao 10 za Ligi Kuu England Msimu huu na kushuhudiAa Kiungo wao Nemanja Matic na Meneja wao Jose Mourinho wakitolewa nje ya Uwanja.
Wakicheza Ugenini huko Upton Park, Chelsea walifungwa Bao 2-1 na West Ham na kujikuta wakizidi kudidimia mkiani mwa msimamo wa Ligi.
West Ham walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 17 kupitia Mauro Zarate lakini kabla ya Haftaimu Kiungo wao Nemanja Matic alipewa Kadi za Njano 2 ndani ya Dakika 9 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wakati wa Haftaimu, Jose Mourinho nae alipewa Kadi Nyekundu kwa kumzonga Refa Jon Moss.

Meneja wa Chelsea alipojipotezea kwa mashabiki wa West Ham baada ya kutolewa nje ya Uwanja kwa kadi!Gary Cahill akipongezwa kwa bao lao la kusawazishaPongezi1-1Andy Carroll akmfunga kipa wa Chelsea bao la pili na mtanange kumalizika kwa West Ham bao 2-1 na kuiwezesha West Ham United  kupanda juu  nafasi ya pili kwa kupata pointi 20.Mauro Zárate akipongezwa kwa bao lake kipindi cha kwanza. West Ham United walianya mabadiliko kipindi cha pili dakika ya 69 kwa kumuingiza Andy Carroll aliyempumzisha Mauro Zárate na dakika ya 79 akawafungia bao la pili kwa kichwa na kufanya 2-0 dhidi ya Chelsea ambao walikuwa wako 10 uwanjani tangu kipindi cha kwanza.Mauro Zárate Dakika ya 17 aliwapa bao la kuongoza West Ham United. Chelsea walisawazishiwa bao na Gary Cahill kipindi cha pili dakika ya 55 na kufanya bao kuwa sare ya 1-1.
Nemanja Matic nje kwa kadi nyekunduJohn Terry na kidole kwa mwamuzi wa kati leo hii baada ya Nemanja Matic kutolewa kwa kadi nyekundu uwanjani.

No comments:

Post a Comment