Cristiano Ronaldo leo hii aliifungia Real Madrid Bao la kwanza wakati iliposhinda Ugenini Bao 3-1 walipocheza na Timu ya Pili kwenye La Liga Celta Vigo.
Bao nyingine za Real zilifungwa na Danilo na Marcelo huku Bao la Celta Vigo likifungwa na Nolito.
Hadi Mapumziko Real walikuwa mbele 2-0 na kilipoanza tu Kipindi cha Pili Gustavo Cabral wa Celta Vigo alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kulambwa Kadi za Njano 2.
Ushindi huu wa Real, ambao bado inawakosa majeruhi Gareth Bale, Karim Benzema na James Rodriguez, umewapaisha na kuwa kileleni Pointi 3 mbele ya Timu ya Pili Celta Vigo na Barcelona.
No comments:
Post a Comment