Bao la Yanga lilifungwa na Juma Abdul dakika ya 9 kwa shuti kali lililowapita mabeki wa Toto katikati na kipa wao na kufanya 1-0.
Dakika ya 45 Yanga walipata penati na penati hiyo kupigwa na Donald Ngoma na kipa wa Toto kuudaka mkwaju huo hivyo Yanga kwenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Toto ya Jijini Mwanza.
Kipindi cha pili dakika ya 48 Simon Msuva aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Abdul aliipatia bao la pili Yanga na kufanya 2-0. Miraji Madenge wa Toto aliwafungia bao kwa kichwa dakika ya 55 na kufanya matokeo kuwa 2-1. Dakika ya 81 Amisi Tambwe aliwapa bao la tatu kwa kufanya 3-1 dhidi ya Toto baada ya kutumia mwanya ambao ulikuwa wazi kwa uzembe wa mabeki wa Toto. Dakika ya 90 Simoni Msuva aliipa Yanga tena bao na mtanange kumalizika kwa bao 4-1.

No comments:
Post a Comment