SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA), zimeipongeza timu ya African Lyon kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu msimu ujao, baada ya kuwa vinara wa Kundi A katika ligi hiyo iliyomalizika juzi.
Wakizungumza na wandishi wa habari kwa nyakati tofauti, Ofisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto na Mwemyekiti wa DRFA Almas Kasongo walisema wainaitakia kila la kheri Africa Lyon katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, kwa kujiandaa vizuri na mikiki mikiki ambayo ina jumla ya timu 16 na kila klabu kucheza michezo 30 kwa msimu, nyumbani na ugenini.
Lyon imefikia hatua hiyo baada ya kushinda mechi 8 na kutoka sare mechi 3 kati ya mechi 14 ilizocheza,na kuiacha nyuma pointi 2 klabu ya KMC FC iliyomaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 25.
Pia Kasongo amezipongeza timu za Ashanti United iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 24, Friends Rangers iliyomaliza katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 23,pamoja na Polisi Dar es salaam iliyomaliza katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 14 zote za Dar es salaam,kwa uthubutu wao wa kujaribu kutinga ligi kuu.
No comments:
Post a Comment