BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 20, 2016

LA LIGA: LEO BARCELONA, ATLETICO MADRID, REAL MADRID...UWANJANI LEO! NANI KUWAONGOZA WENZAKE?

LA LIGA inaingia patamu hii Leo wakati Vigogo wa Spain Watatu wanaowania Ubingwa wote wakiwa kwenye Viwanja Vitatu tofauti wakisaka kutwaa uongozi wa Ligi.
Barcelona, ambao ndio Mabingwa Watetezi na pia Vinara wa La Liga, Leo wako Ugenini kucheza na Deportivo La Coruna.
Atletico Madrid, waliofungana kwa Pointi na Barca, wako pia Ugenini kucheza na Athletic Bilbao.

Real Madrid, ambao wako Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Barca na Atleti, wako kwao Santiago Bernabeu kuivaa Villareal ambayo iko Nafasi ya 4 lakini wako Pointi 15 nyuma ya Real.
Wakati Atleti na Real zipo kwenye wimbi zuri za kuikimbiza na kuifikia Barca hivi karibuni, Barca wao wapo kwenye dhoruba kali iliyowafanya wafungwe Mechi 3 mfululizo za La Liga hadi sasa ambazo
zilifanya walipoteza kabisa pengo lao kubwa la uongozi dhidi ya Atleti na Real.

LA LIGA
RATIBA
Jumatano Aprili 20

21:00 Deportivo La Coruna v Barcelona
21:45 Athletic Bilbao v Atletico Madrid
21:45 Malaga v Rayo Vallecano
21:45 Valencia v SD Eibar
21:45 Sporting Gijon v Sevilla
22:00 Real Madrid v Villareal 


Alhamisi Aprili 21

21:30 Real Sociedad v Getafe
22:00 Granada v Levante
Ijumaa Aprili 22
22:00 Las Palmas v RCD Espanyol

No comments:

Post a Comment