BUKOBA SPORTS

Saturday, May 21, 2016

2015/16 TUNAIKAMILISHA KWA ‘KUIUA’ NDANDA FC



Kikosi cha Mbeya City Fc kesho jumapili kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa kucheza mchezo wa kufungia msimu wa 2015/16 katika ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wageni Ndanda Fc kutoka mkoani Mtwara. Muda mfupi uliopita meneja wa kikosi cha City, Geoffrey Katepa ameidokeza mbeyacityfc.com kuwa nyota wote 18 walitayrishwa kwa ajaili ya kuwakilisha timu yao wako kwenye hari nzuri na tayari kabisa kusaka ushindi mbeya ya timu hiyo kutoka kusini mwa Tanzania.
“Kama unavyoona tumemaliza mazoezi muda huu, yalikuwa ni mazoezi mepesi kueleka mchezo wa kesho kila mmoja yuko vizuri na ana ari kubwa, jambo muhimu kwetu ni kushinda mchezo huo ili tumalize ligi kwa heshima, hatuna wasiwasi wowote tuko salama kwenye msimamo wa ligi, kumaliza kwa ushindi kutatuweka kwenye mapumziko mazuri kwa matayarisho ya msimu mpya”, alisema.


Kuhusu majeruhi Katepa alisema kuwa City itakosa huduma ya nahodha na mlinzi shupavu wa kushoto Hassan Mwasapili alaiye majeruhi kufuatia maaumivu ya nyama za paja yanayomkabili, pia Temi Felix na Deo Julius hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kupisha majeraha waliyonayo.

“Mkuu wa kitengo chetu cha utabibu Dr Joshua kaseko, amenieleza asubuhi kuwa tutawakosa wachezaji hao kutokana na majereha waliyonayo hii ina maana kuwa wataonekana uwanjani wakati wa matayarisho ya msimu mpya, mwalimu tayari kashafanya utaratibu wa wale wataochukua nafasi zao hivyo tuna uhakika wa kuingia uwanjani na kikosi kilicho bora licha ya kutokuwepo kwa nyota hao” alimaliza.

No comments:

Post a Comment