BUKOBA SPORTS

Sunday, May 22, 2016

PEP GUARDIOLA AAGWA RASMI NA BAYERN KWA DFB POKAL YA MIKWAJU YA (PENATI 4-3)

PEP GUARDIOLA amemaliza himaya yake huko Bayern Munich kwa kutwaa Dabo baada ya Jana kutwaa Kombe la Germany, DFB POKAL, walipoibwaga Borussia Dortmund kwa Penati 4-3 Uwanja wa Olimpiki Mjini Berlin.
Hili ni Taji la Pili Msimu huu kwa Bayern ambao pia wamebeba Ubingwa wa Bundesliga kwenye Msimu huu wa mwisho wa Guardiola anaehamia Manchester City na Bayern kutwaliwa na Meneja mpya Carlo Ancelotti.
Kwenye Fainali hii Gemu ilikuwa 0-0 hadi mwisho wa Dakika 90 na Nyongeza ya Dakika 30 haikuzaa Bao.

Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Bayern kushinda kwa Penati 4-3 baada ya Dortmund kupoteza Penati zao 2.
Katika Penati hizo, Douglas Costa ndie alieifungia Bayern Penati ya mwisho na ya ushindi.

Dortmund walikosa Penati zao za Pili na za Tatu pale Kipa wa Bayern, Manuel Neuer, alipookoa ile iliyopigwa na Sven Bender na ile ya Sokratis Papastathopoulos kupaa juu.
Guardiola amedumu Bayern kwa Miaka Mitatu ma kutwaa Ubingwa wa Bundesliga kila Mwaka na kuchukua DFB POKAL mara 2.
Bayern Munich's coach Pep Guardiola and David Alaba celebrate after winning the German Cup

No comments:

Post a Comment