BUKOBA SPORTS

Sunday, May 22, 2016

SERENGETI BOYS WAPATA SARE NYINGINE DHIDI YA MALAYSIA KATIKA MICHUANO YA INDIA


bukobasports.comTimu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys wamepata sare nyingine baada ya Malaysia kusawazisha mabao yote mawili waliyotangulia kufunga vijana hao. Mechi hiyo ni ya michuano ya Kombe la Vijana la AIFF inayofanyika katika mji wa Goa nchini India. Boys walianza kupata bao lao la kwanza katika dakika ya 31 kupitia mshambuliaji wao hatari, Asad Ali Juma na Yohana Oscar akaongeza la pili katika dakika ya 59, ikiwa ni dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Makosa ya walinzi, yaliwaruhusu Malaysia kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika tano tu.

No comments:

Post a Comment