BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 18, 2016

CAF-CC: PUNDE LEO NI YANGA KUUNGANA NA TP MAZEMBE, MO BEJAIA MAKUNDI?

JANA TP Mazembe ya Congo DR na MO Bejaia ya Algeria ziliweza kutinga Hatua ya Makundi ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa faida ya Mabao ya Ugenini na Leo Mabingwa wa Tanzania Yanga wana nafasi nzuri kuungana nao.
Jana TOP Mazembe ilichapwa 2-1 huko Tunisia na Stade Gabesien lakini wamesonga kwa Bao la Ugenini baada ya kushinda 1-0 Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Lubumbashi, Congo DR Wiki 2 zilizopita.
Nao Esperance ya Tunisia imetupwa nje kwa Bao la Ugenini walipotoka Sare ya Nyumbani ya Bao 1-1 na Mouloudia Bejai ya Algeria kufuatia Sare ya 0-0 kwenye Mechi yao ya kwanza.
Leo zipo Mechi 6 na mojawapo ni huko Dundo, Angola ambako Yanga wanarudiana na GD Sagrada Esperanca Timu ambayo waliipiga 2-0 Jijini Dar es Salaam Wiki 2 zilizopita kwa Bao za Simon Anthony na Simon Msuva.
Leo Yanga, wanaohitaji Sare tu au hata wakifungwa 1-0 ili kusonga, wataimarika zaidi kwa kuwemo Kikosini Wachezaji wao Wawili Mapro kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko, ambao hawakucheza Mechi ya Kwanza walipokuwa Kifungoni kutokana na Kadi za Njano.
Mechi hii ya Marudiano hii Leo inatarajiwa kuanza Saa 11 Jioni, Saa za Bongo, na kuchezwa kwenye Estadio Sagrada Esperanca mali ya Klabu hiyo ya Angola unaopakia Washabiki 8,000 na ambao uko Mji wa Dundo ulioko Kaskazini Mashariki ya Angola umbali wa Kilomita 1,134 (Maili 704) kutoka Mji Mkuu wa Angola, Luanda.
Refa wa Mechi hii ni kutoka Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza

YANGA - KIKOSI KILICHOSAFIRI:
MAKIPA: Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’.
MABEKI: Juma Abdul, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Nadir Haroub 'Cannavaro' (Kepteni)
VIUNGO: Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya.
MASTRAIKA: Donald Ngoma, Matheo Anthony, Amissi Tambwe, Paul Nonga
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
RATIBA/MATOKEO
Jumanne Mei 17

(Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2)
Stade Gebasien - Tunisia 2 TP Mazembe - Congo Dr 1 (-2)
ES Tunis - Tunisia 1 MO BAEJAIA - Algeria 1 (1-1)
Leo Jumatano Mei 18
GD Sagrada Esperanca - Angola v Yanga - Tanzania
CF Mounana - Gabon v ES Sahel - Tunisia
Medeama - Ghana v Mamelodi Sundowns - South Africa
Misr Almaqasa - Egypt v Al Ahli - Libya
Marrakech - Morocco v El Merreikh - Sudan
FUS Rabat -Morocco v Stade Malien de Bamako - Mali

No comments:

Post a Comment