BUKOBA SPORTS

Sunday, May 22, 2016

JOSE MOURINHO NA MANCHESTER UNITED HABARI ZAANZA KUPAMBA MOTO.


MABINGWA WAPYA wa FA CUP Manchester United wanatarajiwa wakati wowote ule kumtangaza Jose Mourinho kuwa Meneja wao mpya.
Habari hizi zimepamba moto kwenye Ulimwengu wa Soka lakini, kama kawaida yao, Klabu ya Man United haijatoa tamko lolote.
Jana Meneja wa sasa Louis van Gaal aliiongoza Timu yake huko Wembley Stadium Jijini London kubeba kwa mara 12 FA CUP walipoichapa Crystal Palace kwa Bao la ushindi la Dakika ya 110 la Jesse Lingard ambalo lilifungwa huku Man United wakiwa Mtu 10 baada ya Chris Smalling akiwa ametolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 105.
Licha ya ushindi huo, kuikosa Nafasi ya kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI ndiko kunaonekana kumgharimu Van Gaal Umeneja kama vile alivyotimuliwa David Moyes Mwaka 2014.Lakini zipo habari kuwa Van Gaal atabakia Old Trafford kwa Mwaka wake Mmoja uliobakia katika Mkataba wake akishika wadhifa wa Mkurugenzi wa Soka na kufanya kazi pamoja na Meneja Mourinho ambae hana kibarua tangu aondoke Chelsea Mwezi Desemba.Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Van Gaal na Mourinho kufanya kazi pamoja kwani walikuwa pamoja huko FC Barcelona wakati Van Gaal akiwa Kocha Mkuu na Mourinho Msaidizi wake.
Ferguson na Van Gaal

No comments:

Post a Comment