
Mratibu wa mashindano ya Miss Mbeya 2016 Tom Chilala akifafanua jambo kwa wanahabari waliohudhuria kikao cha maandalizi kilichofanyika katika Hoteli yaBeaco jijini Mbeya
Washiriki wa shindano la walimbwende la Miss Mbeya City 2016 wakiwa katika pozi wakati wa kikao cha mratibu wa mashindano hayo yatakayofanyika Ijumaa(Mei 20) Tom Chilala na wanahabari.
Washiriki wa shindano la walimbwende la Miss Mbeya City 2016 wakiwa katika pozi wakati wa kikao cha mratibu wa mashindano hayo yatakayofanyika kesho Ijumaa(Mei 20) Tom Chilala na wanahabari.
MRATIBU wa Shindano la kumsaka mrimbwende wa kuuwakilisha Mkoa wa Mbeya katika kumsaka miss Tanzania 2016, Tom Chilala amejinasibu taji hilo kunyakuliwa na mrembo kutoka Mbeya.
Aidha shindano hilo linalotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Paradise jijini Mbeya linatarajia kuwashirikisha Warembo 11 kati ya 15 waliojitokeza kuwania taji la Miss Mbeya 2016 watapanda jukwaani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Tom Chilala alisema anajivunia rekodi ya kuandaa mashindano hayo mahali tofauti na washindi wake huchukua taji hilo la Tanzania.
Alisema awali waliojitokeza katika kinyang`anyiro hicho walikuwa warembo 15 kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya lakini ulifanyika mchujo wa awali na kubakia warembo 11 ambao ndiyo watapanda jukwaani.
Alisema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia fedha tasilimu Sh 700,000,wa pili Sh400,000,wa tatu Sh300,000 na mshindi wa nne Sh200,000 huku wa tano hadi wa 11 watapata kifuta jasho Sh 80,000.
Alisema shindano hilo mwanamuziki chipukizi anayetamba kwa sasa katika muziki wa Bongo Fleva Rajabu Abdulkhali (Harmonizer) anatarajia kutumbuiza na kwamba mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
Chilala amewataja warembo watakaopanda jukwaani ni pamoja na Emiliana Abdalah,Anitha Parick,Aziza Lyasamuya na Praxeda Geofrey.
Wengine ni Juliana Gilbert,Nancy Matta,Agnes Boliva,Julitha Mponela,Afrodisia Chapa,Eunice Robert,Pricar Mengi na Juliana Lyampawe.
Kwa upande wao baadhi ya warembo watakaoshindana walijinasibu kuwa mmoja wao atakayepita kutoka Mbeya ndiye atakayenyakua taji hilo kutokana na sifa walizonazo.
No comments:
Post a Comment