Mwendesha pikipiki akiendesha chombo hicho huku akiwa hajavaa kofia ngumu (Helment) kichani muda mfupi kabla ya kupinda kona na kurudi alikotoka wakati akiwakwepa askari wa usalama barabarani waliokuwa wakikamata waendesha pikipiki wasiozingatia sheria za usalama barabara eneo la tuta la stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro.
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kupitia askari wa kitengo cha usalama barabara wamekuwa wakiendesha operesheni ya kukamata waendesha pikipiki wasiozingatia sheria za usalama wa barabara.
Chini pichani mwendesha pikipiki huyo zikimuonyesha namna alivyofanikiwa kukwepa askari ili asikamatwe na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani kwa moja ya sheria hizo ikiwemo ya uvaaji kofia ngumu kichwani inaeleza umuhimu wa uvaaji wa kofia ngumu kichwani hutoa kinga madhubuti endapo dereva wa pikipiki na abiria wake wanaweza kupata ajali na kusaidia kichwa kisiweze kupata madhara.
Askari hao wamekuwa wakikamata makosa ya madevera pikipiki ikiwemo dereva asiyekuwa na leseni, kuvaa kofia ngumu dereva na abiria, bima na upakiaji hatarishi yaani abiria zaidi ya mmoja (mishikaki).
Dereva wa pikipiki akiwa amepakia abiria huku yeye akiwa amejikinga na kofia ngumu kichwa na kofia nyingine iliyopaswa kuvaliwa na abiria ikiwa inaning'nizwa katika chomo hicho.
No comments:
Post a Comment