FAINALI ya EUROPA LIGI ya Mwaka 2016 imechezwa huko St. Jakob-Park Mjini Basel Nchini Uswisi wakati Liverpool ilipoyeyuka Kipindi cha Pili na kutandikwa Bao 3-1 na Sevilla ambao sasa wamekuwa Klabu ya kwanza tangu Bayern Munich itwae Mataji Matatu mfululizo ya Ulaya.
Kati ya Mwaka 1974 na 1977, Bayern Munich ilitwaa Kombe la Ulaya mara 3 mfululizo na Jana Sevilla imeingia Vitabu vya Historia kwa kutwaa EUROPA LIGI kwa Miaka Mitatu mfululizo tangu 2014.
Ushindi huu umeifanya Sevilla sasa kuingizwa kucheza Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao nafasi ambayo walikuwa hawana kwani kwao kwenye La Liga walikosa nafasi hiyo kwa kumaliza Nafasi za chini.
Lakini Kipindi cha Pili waliyeyuka kwenye Mechi na kupigwa Bao 3 za Dakika za 46, 64 na 70 kupitia Kevin Gameiro na mbili za Andujar Moreno.
Hii ni Fainali ya Pili chini ya Jurgen Klopp kwa Liverpool kufungwa Msimu huu baada ya Mwezi Februari kubwagwa kwa Penati na Manchester City kwenye Fainali ya Capital One Cup.
Liverpool akiba: Ward, Benteke, Henderson, Lucas, Allen, Origi, Skrtel
Sevilla walioanza XI: Soria, Mariano, Rami, Carrico, Escudero, Krychowiak, Nzonzi, Coke, Banega, Vitolo, Gameiro
Sevilla akiba: Sergio Rico, Kolodzieczak, Iborra, Cristoforo, Pareja, Konoplyanka, Llorente
No comments:
Post a Comment