BUKOBA SPORTS

Saturday, June 4, 2016

COPA AMERICA CENTENARIO 2016, WENYEJI WAANZA MASHINDANO KWA KICHAPO


MASHINDANO ya Copa Amerika yameanza alfajiri ya kuamkia leo, na kushuhudia wenyeji wa michuano hiyo, Marekani wakianza vibaya baada ya kufungwa mabao 2-0 na Colombia.

Mchezo huo ulianza kwa kasi na kumilikiwa zaidi na Colombia ambao iliwachukuwa dakika 8 tu kupata bao la kwanza lililotokana na uzembe wa walinzi wa Marekani kushindwa kuokoa mpira wa kona iliyopigwa na Edwin Cardona's na kumkuta Christian Zapata na yeye bila ajizi akautia nyavuni.

Marekani walijitahidi kusawazisha bao na dakika ya 36 Clint Dempsey alikosa bao baada ya shuti lake kuokolewa na golikipa Aspira, mpira huo ulisababisha Colombia kufanya shambulizi la kushtukiza na katika harakati za kuokoa mlinzi wa Marekani Yedlin akaunawa mpira na mwamuzi Roberto Gacia toka Mexico akaamuru upigwe mkwaju wa penati.

Wachezaji wa Marekani pamoja na kocha wao Jurgen Krinsman walijaribu kugomea penati hiyo kwa kumzonga mwamuzi lakini haikusaidia maana refa ndiye mwenye maamuzi ya mwisho na kiungo wa Real Madrid James Rodriguez akaukwamisha mpira kimiani kiufundi na kufanya ubao usomeke 2-0.

Kipindi cha pili Marekani walijitahidi angalau kupata hata bao la kufutia machozi lakini bahati haikuwa yao maana dakika ya 58 Clint Dempsey alipiga kichwa mpira wa kona na kumpita kipa Aspina lakini mpira huo uliokolewa kwenye mstari na mlinzi Perez.

Patashika hiyo itaendelea leo kwa michezo mitatu
COSTA RICA vs PARAGUAY
BRAZIL vs EQUADOR
HAIT vs PERU

No comments:

Post a Comment