Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu kwenye ukumbi wa Hotel ya Optima iliyopo Bunazi Misenyi ambapo chama hicho kilichokuwa kinaongozwa na Wajumbe 22 kumteua Jamal Emil Mlinzi ambaye pia ni RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukiongoza chama hicho kwa mara nyingine kwa kura za Ndiyo 21 kati ya 22.
Akiongea na Mtandao huu wa Bukobasports amesema kwa sasa wameanza na mkakati wa kuboresha Uwanja wa Kaitaba kwa kuuwekea Nyasi bandia na kuongeza idadi ya Majukwaa ili uweze kutumika kwa Michezo ya Kimataifa. Pia Chama cha mpira wa miguu Mkoa kimeomba Viwanja kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo na Uwanja wa kwa Ufadili wa FIFA jambo ambalo kimsingi linawezekana kila Mtu akitimiza wajibu wake.
Pamoja na hayo aliomba kupitia mkutano huo kuviomba Vyama vyote vya Wilaya kuomba maeneo ya kujenga Viwanja vya mpira wa miguu kwenye Halmashauri zao husika.
Mwisho aliwashukuru wote kwa nafasi zao na kuwaomba ushirikiano wa hali na mali ili Mkoa wa Kagera uweze kuongeza Timu zingine katika Ligi kuu Vodacom na Madaraja mengine.
Didas Zimbihile alitetea nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu klabu wa TFF kwa kukusanya kura zote 22.
Malinzi amekuwa Mwenyekiti wa KRFA tangu Machi 17, mwaka 2012 na katika kipindi chake cha kuwa madarakani, amesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha hamasa ya soka Kimkoa.
Aidha, Malinzi amesaidia ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba, ambao sasa una mwonekano mzuri, ukiwa unapambwa na nyasi bandia.
No comments:
Post a Comment