BAO la Dakika ya 89 la Diego Costa limewapa ushindi Chelsea katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England chini ya Meneja mpya Antonio Conte walipoifunga West Ham Bao 2-1 Uwanjani Stamford Bridge.
Chelsea walitangulia kufunga katika Dakika ya 47, Kipindi cha Pili, kwa Penati iliyotolewa kufuatia Michail Antonio kumchezea Rafu Cesar Azpilicueta.
West Ham walisawazisha Dakika ya 77 kupitia James Collins lakini Chelsea wakanyakua ushindi kwa kupitia Costa aliepiga kutoka Mita 20.
Hata hivyo Costa alinusurika kuendelea kwenye Mechi hii hadi wakati huo kwani alilambwa Kadi ya Njano mapema na kisha kubahatika kutopewa Kadi ya pili baada ya kumkwangua Mguuni Kipa Adria.
No comments:
Post a Comment