
Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mbaraka Yusup bao la tatu leo kwenye mtanange wa VPL uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Kagera Sugar wamepanda juu nafasi ya Tatu kwenye Msimamo wa VPL baada ya kuwanyuka bao 3-1 Timu ya Ruvu Shooting.
Bao la kwanza la Kagera na la kusawazisha limefungwa na Temi Felix kipindi cha pili baada ya kuongeza kasi, Bao alilolifunga kwa shuti kali kwa mpira wa adhabu. Bao la pili lilifungwa na Seleman Mangoma na la tatu likafungwa na Mbaraka Yusuf. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Sehemu ya Benchi la Timu ya Kagera Sugar.

Kipindi cha pili Tem Felix aliisawazishia bao Kagera Sugar na Kisha baadae Seleman Mangoma akapachika bao la pili na kufanya Kagera Sugar waongoze kwa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting.

wenyeji Kagera Sugar.

Waamuzi wa Mtanange kati ya Kagera Sugar V Ruvu Shooting wakati wa mapumziko wakitoka Nje ya Uwanja kwenda kwenye mapumziko ya dakika chache kujiandaa na dakika 45 za kipindi cha pili. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
No comments:
Post a Comment