Jorge Mendes, Wakala wa Ronaldo, ametoboa habari hizo na pia kusema Mshahara wa Ronaldo, mwenye Miaka 31, ungekuwa ni Pauni Milioni 85 kwa Mwaka lakini Staa huyo hakupendezewa na Ofa hiyo.
Akiongea na Sky Italia Mendes alisema: “Kutoka China wametoa Ofay a Euro Milioni 300 [Pauni Milioni 257] kwa Real na zaidi ya Pauni Milioni 100 kwa Mwaka kama Mshahara kwa Mchezaji! Lakini Fedha sio kila kitu. Real ndio Maisha yake!”
Habari hizi zimefichuka mara tu baada ya kuthibitika kwa Carlos Tevez kuhamia Klabu ya China by Shanghai Shenua na kumfanya awe ndio Mchezaji anaelipwa Mshahara wa juu kabisa Duniani.
Kwa mujibu wa Mendes, Ofa hiyo ya Ronaldo inngemfanya Ronaldo apate Mshahara wa Pauni Milioni 1.6 kwa Wiki na pia Ada ya Uhamisho ingevunja ile Rekodi ya Uhamisho ya Pauni Milioni 89 ambayo Man United waliilipa Juventus kwenye Uhamisho wa Paul Pogba mwanzoni mwa Msimu.
Mendes ameeleza: “Soko la China ni jipya. Wanaweza kununua Wachezaji wengi lakini haiwezekani kwa Ronaldo kwenda huko. Cristiano ni Mchezaji Bora Duniani na ni Bora kupita wote. Ofa za aina hii hutokea!”
No comments:
Post a Comment