Chelsea wamepaa Pointi 9 juu kwenye EPL, Ligi Kuu England, baada kuichapa Bournemouth huku Arsenal wakishinda mwishoni na kushika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi sawa na Liverpool walio Nafasi ya Pili wakati Manchester United wakiiwasha Sunderland na kuifikia kwa Pointi Timu ya 5 Tottenham.
Huko Stamford Bridge, Chelsea wamejizatiti kileleni kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Bournemouth kwa Bao za Pedro, Bao 2, na Penati ya Eden Hazrad.
Ushindi huu wa Chelsea ni wa 12 mfululizo kwenye EPL kwa Klabu hiyo na kujiwekea Rekodi yao wenyewe.
No comments:
Post a Comment