BUKOBA SPORTS

Friday, January 13, 2017

AFCON 2017: FAINALI KUANZA LEO JUMAMOSI, WENYEJI GABON vs GUINEA-BISSAU, BURKINA FASO vs CAMEROON

MASHINDANO ya 31 ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yataanza leo Jumamosi Januari 14 huko Gabon kwa Wenyeji hao kuivaa washiriki wa mara ya kwanza kabisa Guinea-Bissau katika Mechi ya Kundi A.
Nchi 16 zilizogawanywa Makundi Manne ya Timu 4 kila moja zitashirriki michuano hii ambayo Fainali yake itakuwa Februari 5 na kuchezwa kwenye Viwanja Vinne vya Miji ya Libreville, Franceville, Oyem na Port Gentil huko Gabon.
Mashindano haya, ambayo yalichezwa kwa mara ya kwanza Nchini Sudan Mwaka 1957 na kushirikisha Nchi 3 tu na Egypt kutwaa Ubingwa, yatakuwa Na Mechi 32 ndani ya Siku 23 huu Mshindi, atakaepatikana kwenye Fainali Februari 5, akizoa kitita cha Dola Milioni 4.

MAKUNDI:
KUNDI A:
Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea-Bissau
KUNDI B:
Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
KUNDI C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo
KUNDI D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda

WENYEJI:
Hii itakuwa mara ya pili kwa Gabon kuwa Wenyeji wa AFCON kwani Miaka Mitano iliyopita wao na Equatorial Guinea ndio walikuwa Wenyeji na safari hii kufanikiwa tena Uenyeji baada ya CAF kuiondoa Libya, iliyopaswa kuwa Wenyeji 2013, kutokana na Vita na Mwaka huo kuchezwa Afrika Kusini waliotakiwa kuwa Wenyeji wa Mwaka 2017.
Gabon, Nchi ya Watu Milioni 1 Laki 8, ipo Nafasi ya 108 katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani ingawa wanae mmoja wa Mastraika hatari Duniani Pierre-Emerick Aubamenyang anaecheza Bundesliga huko Germany na Klabu ya Borussia Dortmund.

WACHEZAJI MVUTO:
Mbali ya Aubameyang, macho ya wengi yatawafuatilia Mchezaji Bora Afrika Riyad Mahrez wa Mabingwa wa England Leicester City anaechezea Algeria na Sadio Mane wa Liverpool anaecheza Senegal.
Pia wapo Wachezaji wengine 23 wanaocheza EPL, Ligi Kuu England, na hao ni pamoja na Sentahafu wa Manchester United Eric Bailly wa Mabingwa Watetezi Ivory Coast, Fowadi wa West Ham wa Ghana Andre Ayew, wa Leicester Islam Slimani anaecheza Algeria na Winga wa Crystal Palace atakaecheza Ivory Coast Wilfried Zaha.

Zaha ameamua kuichezea Ivory Coast hivi Juzi tu baada ya kuwahi kuzichezea Timu za Vijana za England na Majuzi kufunga Bao lake la kwanza kwa Nchi yake walipopasha na Uganda.

Wachezaji wengine mvuto ni yule wa Egypt Mohamed Salah anaecheza Serie A na AS Roma baada kuhama kutoka Chelsea.

Lakini Historia itamgusa Kipa wa Egypt Essam El Hadary ambae anaweza kuweka Rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye Umri kubwa kabisa kuwahi kucheza Fainali za AFCON ikiwa atacheza kwani atatimiza Mika 44 hapo Januari 15.
Egypt ndio Nchi inayomeremeta Afrika kwa kutwaa Ubingwa mara nyingi, mara 7.

KOCHA WA KIHISTORIA:

Mfaransa Herve Renard anawania kuwa Kocha wa kwanza kutwaa Ubingwa wa Afrika mara 3 na Nchi 3 tofauti baada ya kuiongoza Zambia Mwaka 2012 na Ivory Coast katika Mashindano yaliyopita na safari hii yupo na Morocco.
Makocha wengine waliowahi kutwaa Ubingwa wa Afrika mara 3 ni Charles Gyamfi akiwa na Ghana Miaka ya 1963, 1965 na 1982 na Hassan Shehata akiwa na Egypt Miaka ya 2006 na 2010.

VIWANJA:
Viwanja vitakavyotumika ni Stade de l’Amitié huko Libreville, Gabon, unaochukua Watu 38,000, ambako Kundi A ndio litacheza Mechi zake, na kingine cha Kundi B ni Port Gentil Stadium, Port Gentil, wenye kuchukua Washabiki 20,000, Kundi C lipo Stade de Franceville Mjini Franceville wenye uwezo wa Watu 20,000 wakati Kundi D litakuwa huko Oyem Stadium ulioko Assok Ngomo, Gabon, uwezo 20,000.
Mabingwa Watetezi wa Afrika ni Ivory Coast lakini safari hii watawakosa Wachezaji wao wakubwa, wale Ndugu Toure, yaani Yaya na Kolo, ambao wamestaafu, na Majeruhi Yao Gervinho.


MABINGWA WATETEZI:
Ivory Coast walitwaa Ubingwa wa Afrika huko Equatorial Guinea Mwaka 2015.
Wenyeji Gabon wapo Kundi A pamoja na Burkina Faso, Cameroon na Guinea-Bissau iliyotinga Fainali kwa mara ya kwanza.


JIRANI ZETU - UGANDA:
Jirani zetu Uganda wapo kundi D pamoja na Ghana, Mali na Egypt ambao wanarejea kwenye Fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu watwae Ubingwa Mwaka 2010.

AFCON 2017
RATIBA:
Mechi za Makundi
Jumamosi Januari 14
Kundi A

19:00 Gabon v Guinea-Bissau
2200 Burkina Faso v Cameroon

Jumapili Januari 15
Kundi B

19:00 Algeria v Zimbabwe
22:00 Tunisia v Senegal

Jumatatu Januari 16
Kundi C

19:00 Ivory Coast v Togo
22:00 Congo DR v Morocco

Jumanne Januari 17
Kundi D

19:00 Ghana v Uganda
22:00 Mali v Egypt

Jumatano Januari 18
Kundi A

19:00 Gabon v Burkina Faso
22:00 Cameroon v Guinea-Bissau

Alhamisi Januari 19
Kundi B

19:00 Algeria v Tunisia
22:00 Senegal v Zimbabwe

Ijumaa Januari 20
Kundi C

1900 Ivory Coast v Congo DR
2200 Morocco v Togo

Jumamosi Januari 21
Kundi D

19:00 Ghana v Mali
22:00 Egypt v Uganda

Jumapili Januari 22
Kundi A

2200 Cameroon v Gabon
2200 Guinea-Bissau v Burkina Faso

Jumatatu Januari 23
Kundi B

2200 Senegal v Algeria
2200 Zimbabwe v Tunisia

Jumanne Januari 24
Kundi C

2200 Morocco v­­ Ivory Coast
2200 Togo v Congo DR

Jumatano Januari 25
Kundi D
2200 Egypt v Ghana
2200 Uganda v Mali

Robo Fainali
Jumamosi Januari 28

1900 Mshindi Kundi A v Mshindi wa 2 Kundi B
2200 Mshindi Kundi B v Mshindi wa 2 Kundi A

Jumapili Januari 29
1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa 2 Kundi D
2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa 2 Kundi C

Nusu Fainali

Jumatano Februari 1
2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4

Alhamisi Februari 2
2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3

Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4

2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2

Fainali
Jumapili Februari 5
2200 Finalist 1 v Finalist 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

No comments:

Post a Comment