BUKOBA SPORTS

Friday, January 6, 2017

JOHN OBI MIKEL AIAGA CHELSEA KWENDA CHINA, ROMAN AMWAMBIA SAFARI NJEMA!

John Obi Mikel ametangaza kupitia Posti kwenye Mitandao ya Kijamii kuihama Chelsea kujiunga na Klabu ya China inayocheza Supa Ligi Tianjin TEDA.
Mikel, mwenye Miaka 29, alijiunga na Chelsea akiwa na Miaka 19 akitokea Klabu ya Norway Lyn Mwaka 2006 na kucheza Mechi 374.
Lakini Msimu huu, chini ya Meneja Mpya Antonio Conte, Mikel hajacheza hata Mechi moja na hilo limemfanya ahame.
Akiwa na Chelsea, Mikel alitwaa Makombe 11 yakiwemo Mawili ya Ubingwa Ligi Kuu England na moja la UEFA CHAMPIONS LIGI.
Akiaga, Mikel alitoa Shukran kwa Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich pamoja na Mashabiki wa Klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment