BUKOBA SPORTS

Sunday, January 1, 2017

KOCHA WA BAYERN PAUL CLEMENT KUTUA SWANSEA KAMA MENEJA MPYA

Swansea wapo mbioni kumteua Paul Clement kama Meneja wao mpya.
Clement, Bosi wa zamani wa Derby County na sasa yupo Bayern Munich kama Kocha Msaidizi, amekuwa mazungumzoni na Swansea kuwa Meneja wao wa 3 Msimu huu.
Huenda mazungumzo hayo yakakamilika kabla ya Jumanne ambapo Swansea, wakiwa mkiani mwa EPL, Ligi Kuu England, watasafiri kwenda London kucheza na Crystal Palace.

Clement anatarajiwa kurithi nafasi ya Bob Bradley alietimuliwa mara baada ya Swansea kuchapwa 4-1 na West Ham Siku ya Boksing Dei baada kudumu kwa Siku 85 tu.

Clement, mwenye Miaka 44, alikuwemo kwenye usaili uliomteua Bob Bradley na kuvutia kiasi cha Swansea kumtaka yeye sasa achukue nafasi hiyo.
Meneja huyu mtarajiwa amewahi kufanya kazi kama Msaidizi wa Carlo Ancelotti huko
Chelsea, Paris St Germain, Real Madrid na sasa Bayern Munich.

Lakini kazi pekee aliyofanya kama Meneja, huko Derby County, ilitibuka Miezi 8 tu tangu ateuliwe alipotimuliwa Februari 2016 bila kutegemewa kwani aliiweka Derby Nafasi ya 5 baada kuongoza Ligi ya Daraja la Championship Miezi Miwili nyuma.

No comments:

Post a Comment